Ewe baba yangu mdogo, sema: Laa ilaaha illa llaahu (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu) neno ambalo nitakutetea kwalo mbele ya Mwenyezi Mungu
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Saidi Bin Musayyab, kutoka kwa baba yake amesema: Yalipomfika mauti Abuu Twalib, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimjia akamkuta yuko pamoja na Abuu Jahali na Abdallah Bin Umaiyya bin Mughiira, akasema: "Ewe baba yangu mdogo, sema: Laa ilaaha illa llaahu (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu) neno ambalo nitakutetea kwalo mbele ya Mwenyezi Mungu", Abuu Jahali akasema: Hivi unataka kuichukia mila ya Abdul Muttwalib (Yaani baba yake) Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akaendelea kumrejelea neno hilo, nao pia wakirudia kumwambia maneno yao, mpaka Abuu Twalib akasema kwa neno lake la mwisho alilowasemesha: Niko katika mila ya Abdul Muttwalib, na akakataa kusema: Laa ilaaha illa llaah, mpokezi anasema: Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Wallahi (Namuapia Allah) nitakuombea msamaha kwa muda wote madam sijakatazwa, Allah akateremsha: "Haifai wala haitakiwi kwa Nabii na wale walioamini kuwaombea msamaha washirikina" [Attauba: 113], Na akateremsha kuhusu Abuu Twalib, akasema kumwambia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika wewe humuongoi umpendaye, lakini Allah anamuongoa amtakaye" [Al-Qasas:56]
Explanation
Benefits
Kuwaiga mababa na wazee katika batili ni katika vitendo vya watu wa zama za ujinga.
Ukamilifu wa huruma yake Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na pupa yake katika kuwalingania watu na kuwaongoza.
Hili ni jibu kwa watu wanaodai kuwa Abuu Twalib alisilimu.
Matendo huzingatiwa mwisho.
Kubatilika kujifungamanisha na kushikamana na Mtume au mwingine asiyekuwa yeye kwa lengo la kupata kheri na kuzuia madhara.
Atakayesema "Laa ilaaha illa llaah" kwa kuwa na elimu na yakini na kuitakidi kwa dhati juu yake basi atakuwa kaingia ndani ya Uislamu.
Madhara ya watu waovu na marafiki wabaya kwa mwanadam.
Maana ya "Laa ilaaha illa llaah": Ni kuacha ibada za masanamu na wachamungu na watu wema na kumpwekeshea ibada Mwenyezi Mungu peke yake, nakwamba washirikina wanaju maana yake.
Inafaa kumtembelea mgonjwa mshirikina ikiwa anatarajiwa huenda akasilimu.
Uongofu wa kumuafikisha mja afungue moyo wake uko mkononi mwa Allah peke yake hana mshirika, bali jukumu la Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kuongoza kwa kuelekeza, muongozo, na kufikisha ujumbe.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

