“Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, ole wao waarabu na watahadhari dhidi ya shari iliyokaribia, imefunguliwa leo katika ngome ya Ya'juuju na Ma'ajuju upenyo wa kiasi hiki.”
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Zainab bint Jahshi radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliingia ndani kwake akiwa na mfadhaiko huku akisema: “Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, ole wao waarabu na watahadhari dhidi ya shari iliyokaribia, imefunguliwa leo katika ngome ya Ya'juuju na Ma'ajuju upenyo wa kiasi hiki.” Jahshi akasema: Basi nikasema ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Je, tuangamie na hali miongoni mwetu wamo watu wema? Akasema: "Ndio, ikiwa maovu yatakithiri".
Explanation
Benefits
Himizo la kukemea maasi na kuzuia kutokea kwake.
Maangamizo ya watu wote hutokea kwa sababu ya kukithiri kwa maasi na kuenea kwake, na kutoyakemea hata kama watu wema ni wengi.
Majanga huwakumba watu wote, wema na waovu, lakini wao watafufuliwa kulingana na nia zao.
"Amewataja Waarabu katika kauli yake: "Ole wao Waarabu kwa shari iliyokaribia"; kwa sababu wao ndio walioingia katika Uislamu kwa wingi wakati akisema hivyo.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

