Mambo ya kimaumbile ni matano: Kutairi, na kunyoa sehemu za siri, na kupunguza masharubu, na kupunguza kucha na kunyofoa nywele za kwapa
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Mambo ya kimaumbile ni matano: Kutairi, na kunyoa sehemu za siri, na kupunguza masharubu, na kupunguza kucha na kunyofoa nywele za kwapa".
Explanation
La kwanza: Kutairi, nako ni kukata ngozi iliyozidi juu ya kichwa cha dhakari kwa mwanaume, na kukata kingozi katika tupu ya mwanamke juu ya malaha palipo tundu la uke.
La pili: Kunyoa sehemu za siri, nako ni kunyoa nywele za kinena zinazozunguka tupu ya mbele.
La tatu: Kupunguza masharubu, nako ni kupunguza kilichoota juu ya mdomo wa juu wa mwanaume mpaka mdomo uonekane wazi.
La nne: Kupunguza kucha.
La tano: Kunyofoa nywele za kwapa.
Benefits
Sheria ya kushikamana na mambo haya, na kutoghafilika nayo.
Mambo haya yanafaida za kidini na kidunia, miongoni mwake: Kupendezesha muonekanao, na kusafisha mwili, na kujiweka tayari kwa usafi, na kwenda kinyume na makafiri, na kutekeleza amri ya Allah.
Kumetajwa katika hadithi zingine ziada ya jambo jingine la kimaumbile tofauti na matano haya, mfano: Kufuga ndevu, na mswaki na nyinginezo.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

