Ewe Mwenyezi Mungu kwa ajili yako nimejisalimisha, na kwako nimeamini, na juu yako nimetegemea, na kwako nimejisogeza, na kwa ajili yako napambana. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kwa utukufu wako hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa wewe najikinga kwa kuto nipoteza, wewe ndiye uliye hai ambaye hafi, na majini na watu wanakufa
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Na imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu kwa ajili yako nimejisalimisha, na kwako nimeamini, na juu yako nimetegemea, na kwako nimejisogeza, na kwa ajili yako napambana. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kwa utukufu wako hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa wewe najikinga kwa kuto nipoteza, wewe ndiye uliye hai ambaye hafi, na majini na watu wanakufa".
Explanation
Benefits
Ulazima wa kutegemea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake na kuomba hifadhi kutoka kwake; kwa sababu yeye ndiye mwenye kusifika kwa sifa kamilifu, basi yeye peke yake yake ndiye mwenye kutegemewa, na viumbe wote hawajiwezi na mwisho wao ni kifo, hivyo wao hawastahiki kutegemewa.
Kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika dua kwa maneno haya yaliyokusanya kila kitu, na yenye kuzuia kingenecho kuingia humo, yanayoelezea kwa imani ya kweli na yakini ya kiwango cha juu.
Amesema As-Sa'diy: Kauli yake: "Wewe ndiye uliye hai" Yaani: Wewe pekee ndiye unayestahiki kuombwa kinga na si mwingine zaidi yako.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

