Hakika mimi ninajua kuwa wewe ni jiwe, haudhuru wala haunufaishi, na lau kama nisingemuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikubusu basi nisingekubusu
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Omari -radhi za Allah ziwe juu yake-: Ya kwamba siku moja alikuja katika jiwe jeusi akalibusu, kisha akasema: Hakika mimi ninajua kuwa wewe ni jiwe, haudhuru wala haunufaishi, na lau kama nisingemuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikubusu basi nisingekubusu.
Explanation
Benefits
Makusudio ya kulibusu jiwe jeusi ni kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Amesema Nawawi: Maana yake nikuwa halina uwezo wa kunufaisha wala kudhuru, nakuwa hilo ni jiwe lililoumbwa kama viumbe vingine ambavyo havidhuru wala havinufaishi, na akalitangaza wazi hilo Omari katika msimu; ili wakashuhudie waliohudhuria katika miji yao, na walihifadhi toka kwake hilo waliohudhuria katika msimu, wanaotoka katika nchi mbali mbali.
Ibada zote zinasimama katika msingi wa sheria; haifanyiki katika ibada hizo ila ile aliyoiweka Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuwa ni sheria.
Ikithibiti ibada kuwa ni sahihi itatekelezwa hata kama hekima yake haikujulikana; kwa sababu watu kuitekeleza na kutii kwao kwa kuifanyia kazi ni katika hekima zilizotakiwa.
Katazo la kubusu vitu ambavyo sheria haikusema kuwa tuvibusu kwa lengo la kuviabudu, kama mawe na mengineyo.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

