Hakika wanyama hawa wafugwao ni wanyama kama walivyo wanyama pori, watakaokushindeni miongoni mwao (kuwachinja) basi fanyeni hivyo
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Raafi bin Khadiji radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Siku moja tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake maeneo ya Dhul-Hulaifa, watu wakapatwa na njaa, wakapata ngamia na mbuzi, akasema: Na Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa mwisho wa watu wote, wakaharakisha, wakachinja, na wakabandika vyungu, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaamrisha vyungu vikamiminwa, kisha akagawa na akalinganisha mbuzi kumi sawa na ngamia mmoja, ngamia mmoja akatoroka, wakamtafuta, akawashinda, na hawakuweza kumpata, na walikuwa na farasi wachache, mtu mmoja akarusha mshale, Mwenyezi Mungu akauzuia, kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika wanyama hawa wafugwao ni wanyama kama walivyo wanyama pori, watakaokushindeni miongoni mwao (kuwachinja) basi fanyeni hivyo", Raafi akasema: Sisi tunawahofia maadui kesho, na hatuna visu, je tuchinje kwa miti mikavu iliyochongwa? Akasema: "Mnyama yoyote atakayemwagwa damu, na akatajiwa jina la Mwenyezi Mungu basi kuleni, isipokuwa jino na kwato, na nitakuelezeni kuhusu hilo: Ama jino ninamaanisha mfupa, na ama kwato ni visu vya wahabeshi".
Explanation
Benefits
Kiongozi anatakiwa kuwaadabisha raia wake na jeshi lake, kwani aliwaadabisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa haraka hii na maamuzi haya waliyoyafanya, kabla ya kuchukua idhini yake, malipo yao yakawa ni kuwanyima walichokitaka.
Uharaka wa kuitika amri za Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao.
Katazo la kuchukua ngawira mpaka zigawanywe.
Uadilifu hasa hasa katika sehemu ya kupambana na maadui na makafiri; kwa sababu hilo ni miongoni mwa sababu za ushindi na kuwazidi maadui.
Amesema Nawawi: Atakapofuga mtu kuwa ngamia au ng'ombe au farasi anaweza kumdhuru au mbuzi akakimbia au kinginecho basi anakuwa ni sawa kiwindwa kingine, kinakuwa halali kwa kukirushia mshale au kinginecho.
Ni wajibu kumchinja mnyama ili awe halali kuliwa, na mnyama ni sharti: 1- Awe halali kuliwa, 2- Awe anawezekana kupatikana, ama asiyewezekana hukumu yake ni sawa na hukumu ya wanyama pori, 3- Awe ni mnyama wa nchi kavu; ama wanyama wa Baharini hao si sharti kuchinjwa.
Sharti za kusihi kuchinja: 1- Mchinjaji awe na vigezo vya kuchinja, kwa kuwa na akili, na utambuzi, na awe muislamu au Ahlu kitab, 2- Ataje jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kuanza kuchinja, 3- Kifaa cha kuchinjia kiwe chenye kufaa, yaani kifaa kinachotumika kuchinjia kiwe kikali cha madini ya aina yoyote ile isipokuwa mfupa na kwato, 4- Kuchinja kuwe mahala pa kuchinjia kwa mnyama anayewezekana kuchinjwa, kwa kukata mshipa wa fahamu na koo na mishipa ya shingo.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

