Nimeamrishwa nisujudu kwa viungo saba
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao -kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu-Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - amesema: "Nimeamrishwa nisujudu kwa viungo saba, kwa paji la uso, na akaashiria kwa mkono wake katika pua yake, na mikono miwili na magoti mawili, na ncha za miguu miwili, na wala tusizikunje nguo na nywele".
Explanation
Cha kwanza: Paji la uso: Nao ni ubapa wa uso ulioko juu ya pua na macho mawili, Na akaashiria -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa mkono wake katika pua yake, akieleza kuwa paji la uso na pua ni kiungo kimoja katika vile saba, na akitia msisitizo kwa mwenye kusujudu kuwa agusishe pua yake katika ardhi.
Cha pili: na cha tatu: Ni mikono miwili.
Cha nne na cha tano: Ni magoti mawili.
Cha sita na cha saba: Ni vidole vya miguu miwili.
Na akatuamrisha tusizifunge nywele zetu, au kuzikunja kunja nguo zetu katika ardhi wakati wa kusujudu kwa kuilinda ardhi (Isiguse paji la uso); bali tuziache mpaka zidondoke katika ardhi, ili zisujudu pamoja viungo.
Benefits
Karaha ya kukusanya nguo na nywele ndani ya swala.
Ni wajibu kwa mwenye kuswali atulizane ndani ya swala yake, na hii ni kwa kuweka viungo saba vya kusujudu juu ya ardhi, na atulizane hapo mpaka alete dua zote zilizopangwa na sheria.
Katazo la kufunga nywele hili ni maalumu kwa wanaume pasina wanawake; kwa sababu mwanamke ndani ya swala ameamrishwa kujisitiri
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

