Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akifungua swala kwa takbira (Allaahu Akbaru) na kisomo kwa kuanza na Alhamdulillaahi Rabbil a'alamiin
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akifungua swala kwa takbira (Allaahu Akbaru) na kisomo kwa kuanza na Alhamdulillaahi Rabbil a'alamiin, na alikuwa anaporukuu hanyanyui wala hainamishi kichwa chake, lakini kati na kati, na alikuwa anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu hasujudu mpaka alingane wima, na alikuwa anaponyanyua kichwa chake kutoka katika sijida hasujudu mpaka alingane sawa kwa kukaa, na alikuwa akisoma tahiyatu kila baada ya raka mbili, na alikuwa akiutandika mguu wake wa kushoto na kuusimamisha mguu wake wa kulia, na alikuwa akikataza mkao wa Shetani, na akikataza mtu kulaza mikono yake kama wanyama wakali, na alikuwa akihitimisha swala kwa salamu
Explanation
Benefits
Uwajibu wa takbira ya kuhirimia swala, inayoharamisha kila kauli au kitendo kinachopingana na kauli za swala na vitendo vyake, na kwamba kinyume na namna hiyo hakuna namna nyingine inayofaa kuingia ndani ya swala.
Uwajibu wa kusoma Suratul Faatiha.
Uwajibu wa kurukuu, na jambo bora zaidi ndani yake ni kulingana sawa, bila kuinuka, wala kuinama.
Uwajibu wa kuinuka kutoka katika rukuu, na uwajibu wa kulingana sawa katika kisimamo baada yake.
Uwajibu wa kusujudu, na uwajibu wa kunyanyuka kutoka katika kusujudu, na kulingana sawa wakati wa kukaa baada yake.
Sheria ya kulaza mguu wa kushoto kwa mwenye kuswali na kusimamisha mguu wa kulia katika kukaa ndani ya swala, ama katika tahiyatu ya mwisho katika swala ambayo ina tahiyatu mbili kama Magharibi na Ishaa, sheria ni kukalia kalio moja (Tawaruku), na zimekuja hadithi zingine kuhusu hilo.
Katazo la kujifananisha na Shetani katika kukaa kwake, na hiyo ni mtu kukaa juu ya makalio yake na kulaza miguu yake juu ya Ardhi, au akaisimamisha na akakaa kati kati yake ikiwa katika Ardhi.
Katazo la kujifananisha na wanyama washambuliao katika kutandaza mikono yake, nayo ni kutandaza mikono yake mwenye kuswali katika Ardhi, kwani hilo ni ishara ya uvivu na udhaifu.
Katazo la kujifananisha na Shetani na wanyama katika vitendo vyao.
Uwajibu wa kuhitimisha swala kwa salamu, nayo ni dua kwa wenye kuswali na waliohudhuria na wema wasiokuwepo kwa kuwaombea amani dhidi ya kila shari na mapungufu.
Uwajibu wa kutulizana ndani ya swala.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

