Asistanji mmoja wenu kwa chini ya mawe matatu
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Salman radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Washirikina walisema kutuambia: Hakika mimi ninamuona jamaa yenu anakufundisheni kila kitu, mpaka anakufundisheni kukidhi haja, akasema: Ndiyo, hakika yeye ametukataza kustanji mmoja wetu kwa mkono wake wa kulia, au kuelekea kibla, na akakataza kinyesi cha wanyama na mifupa, na akasema: "Asistanji mmoja wenu kwa chini ya mawe matatu".
Explanation
Benefits
Kumebainishwa baadhi ya adabu za msalani na kustanji.
Uharamu wa kuelekea kibla wakati wa kukidhi haja ndogo au kubwa; kwa kauli yake: "Alitukataza" Na asili ya katazo ni uharamu.
Katazo la kustanji, au kutumia maji kwa mkono wa kulia; kwa sababu ya kuuheshimu.
Ubora wa mkono wa kulia kwa mkono wa kushoto; kwa sababu mkono wa kushoto hutumika kuondoa najisi na uchafu, na wa kulia ni kinyume na hivyo.
Uwajibu wa kuondoa najisi kwa maji au mawe, sawa sawa najisi iwe kidogo au nyingi.
Katazo la kustanji kwa chini ya mawe matatu; kwa sababu mawe chini ya matutu huwa hayatakatishi mara nyingi.
Kila kinachotimiza lengo la kujisafisha na kujitakatisha, basi kinafaa, bali alitaja mawe rehema na amani ziwe juu yake; kwa sababu ndio hutumika mara nyingi, na kila kitakachokuwa hivyo basi hakina maana.
Mapendekezo ya kuhitimisha kustanji kwa witiri, ikiwa kutakata kutakuwa kwa mawe manne basi itapendeza aongeze la tano, na hivyo hivyo; kwa kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayestanji kwa mawe basi na afanye witiri".
Katazo la kustanji kwa kinyesi cha wanyama: ima ni kwakuwa ni najisi, au kwakuwa ni malisho ya wanyama wa Majini.
Katazo la kustanji kwa mifupa; kwakuwa ima ni najisi, au ni chakula cha majini wenyewe.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

