Zakah ni Aina Mbili الزكاة

Ubao kuhusu zakat, iliyoandikwa na Sheikh Heitham Sarhaan,

Ametaja Mas'ala muhimu kuhusu zakat ya wajib na ya sunnah,
Na maana ya zakat, na Mali ambayo zakat ni wajib,

Na wanaopewa zakat, pamoja na Ahkam muhimu ya fiqhi kuhusu zakat katika ubao moja.

#Zaka_ya_Fitr
زكاة الفطر
Vipi utasafisha swaumu yako kutokana na upungufu na uchafu?
Vipi utaingiza furaha mioyoni mwa masikini na wahitaji ili wafurahie Eid kama unavyofurahi wewe?

📖 Tafakari athari hii:
Kutoka kwa Ibn Abbas (Radhi za Alla ziwe juu yao) amesema:
«Amefaradhisha Mtume wa Allah (Swalla Allaahu alayhi wa sallam) Zaka ya Fitr kama utakaso kwa aliyefunga kutokana na maneno machafu na matendo mabaya, na kama chakula kwa masikini».

🕌 Na Zaka ya Fitr ni wajibu kwa kila Muislamu kwa nafsi yake, na kwa wale anaowajibika kuwatunza kama mkewe na watoto wake, ikiwa anamiliki zaidi ya chakula chake na chakula cha familia yake kwa siku hiyo.
Hivyo, haishurutishwi kumiliki kiasi maalum cha mali.

🌾 Na kiasi kinachowajibika kwa kila mtu ni pishi moja ya kila nafaka na tunda ambalo watu hulitumia kama chakula, kama vile tende, mchele na dengu.
Kutoka kwa Ibn Umar (Radhi za Allah ziwe juu yao) alisema:
«Amefaradhisha Mtume wa Allah (Swalla Allaahu alayhi wa sallam) a Zaka ya Fitr pishi moja ya tende au shayiri, kwa mtumwa na aliye huru, mwanamume na mwanamke, mdogo na mkubwa miongoni mwa Waislamu».
Na akaamrisha itolewe kabla ya watu kwenda kuswali.

⏳ Na inawajibika kwa kuzama kwa jua la siku ya mwisho ya Ramadhani.
Na bora zaidi ni kuitoa kabla ya swala ya Eid.
Na hakuna ubaya kuitoa kabla ya Eid kwa siku moja au mbili, yaani kuanzia usiku wa ishirini na nane, kwa sababu mwezi unaweza kuwa na siku ishirini na tisa au thelathini.

❗ Na haijuzu kuichelewesha baada ya swala ya Eid, na yeyote asiyeitoa siku ya Eid anapata dhambi isipokuwa kama ana udhuru, na ni lazima ailipie.

🤲 Hivyo, fanya haraka kuitoa kwa moyo safi na kwa kutafuta radhi za Allah.

 

Shopping Basket