من نحن؟
اللغة السواحلية Kiswahili
📌 Bango zuri la utambulisho wa da‘wah lenye kichwa “Sisi ni nani?”, limeundwa kuwafahamisha wageni kuhusu ukweli wa Uislamu, itikadi yake, ujumbe wake, na maadili yake, pamoja na kueleza nafasi ya msikiti na ukaribisho wake kwa wote, Waislamu na wasiokuwa Waislamu.
📖 Lina majibu mafupi na wazi kuhusu Uislamu, maelekezo ya kutembelea, pamoja na msimbo wa QR kwa ajili ya kupata vyanzo vya kuaminika kwa haraka.
🕌 Linafaa kuwekwa katika misikiti, vituo vya Kiislamu, na maonyesho ya da‘wah, ili liwe njia tulivu na ya kuvutia ya kuutambulisha Uislamu kwa wasiouzungumza Kiarabu na wageni wapya.
#Dawah #Uislamu #Misikiti #JifunzeKuhusuUislamu #WelcomeToIslam
🌐 sarhaan.com
من نحن؟
اللغة السواحلية
Sisi ni nani?
Sisi ni waislamu, tunaabudu Allah peke yake hana shirika yeyote, na tunafuata Qurani Tukufu na sunnah ya mtume صلى الله عليه وسلم kwa ufahamu wa sahaba Allah awe radhi nao.
Uislamu ni dini ya tawheed, inalingania watu kuabudu Allah peke yake, na kukuwa na huruma, na uadilifu na tabia njema.
Tunaamini ya kuwa:
- Allah ni mmoja hana shirika yeyote.
- Qurani ni maneno ya Allah.
- Mtume Muhammad صلى الله عليه وسلم ni mtume wa mwisho.
- Tunaamini kwa nabi wote kama vile Ibrahim, Musa, Issa ibn maryam, tunawapenda wote, tunaamini kwa risala zao.
- Tunaamini kuna siku ya kufufuliwa na siku ya hesabu na jannah na moto wa jahanam.
Lengo letu ni Kuabudu Allah na kufaidi jamii. manhaj yetu ni ya ukati na uadilifu.
Tunalingania watu kwa tabia njema, huruma, uadilifu na kuishi vyema na kila mtu.
Na tunakata kuvuka mpaka katika dini na vurugu na uvamizi.
Tunaheshimu kanuni za sheria katika nchi tunayokaa, na tunafanya bidii kukuwa watu wema wanaofaidi jamii.
____
Kuhusu msikiti:
Msikiti ni pahala safi na tukufu na bora katika ardi, na ni nyumba zilizojengwa kuabudu Allah peke yake.
Msikiti sio miliki ya mtu yeyote bali ni ya Allah, ni wazi kwa yeyote anayetaka kuabudu Allah au kujua kuhusu uislamu au kurudi kwa Allah.
Tunafurahi kupokea swali zenu kwa heshima za dhati.
_
Je asiyekuwa muislamu anaeza ingia msikitini?
Ndio, tunawakaribisha katika ziara yenu ya kutaka kujua kuhusu uislamu.
Munaeza fanya ziara wakati wowote kwa kupitia idara ya msikiti au kupitia aliyekuwa na cheo ya kupokea wanaofanya ziara, na sana sana :
- wakati wa salah.
- katika jumamosi na jumapili ambazo ni siku ya kupokea wanaofanya ziara.
- katika Eidul fitr na Eidul adha.
- wakati wa kupatiana iftar mwezi wa Ramadan.
Msikiti ni mahala ya kufanya ibadah, kuelemishana na usalama.
_
Maelekezo ya kufanya ziara:
- Yafaa kuzingatia na kuheshimu mahala hapa kwani ni nyumba miongoni mwa nyumba za Allah.
- Ni wajibu kutoa viatu kabla kuingia chumba cha kusali.
- Kuna mahala iliyowekwa kwa wanawake kuingia na kusali.
- kuna nguo nzuri za kuvaa kama kuna haja wakati wa kufanya ziara.
__
Kutaka kujua zaidi kuhusu Uislamu au kutaka nakala ya Qur'an:
https://sarhaan.com/
Karibuni.